2025 ENENDA KWA UWEZO WAKO HUU.
Shalom shalom, heri ya mwaka mpya 👋. Karibu tujifunze pamoja na ROHO WA MUNGU ATUSAIDIE.
Leo ntaongea na mtu anayetaka kufanya biashara, kuanza masomo, kuanza ujenzi, kuanza ndoa .kuanza huduma - kazi ya MUNGU, na wewe unayetamani kufanya Jambo ambalo lilishindikana kwako mwaka jana. .
Siku moja MUNGU a limwambia Yeremia; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa; Yeremia akaanza kujitetea kwamba hawezi kusema na pia yeye ni mdogo, sikiliza majibu ya MUNGU kwa Yeremia; ( utakwenda kwa kila mtu nitayekutuma kwakwe)
Kumbe kwa neno la MUNGU mwaka huu 2025 tutafanya mambo makubwa ambayo kwa akili zetu mwaka jana 20 24 tuliona hatuyawezi, uliona hauwezi kufanya biashara kwa mtaji wako mdogo,uliona hauwezi kujenga nyumba kwa kipato chako kidogo, uliona hauwezi kuendelea na msomo kwa mshahara weko mdogo, uliona hauwezi kufanya mambo makubwa kwa umri wako mdogo, uliona hauwezi kumtumikia MUNGU kwa mtaji wako mdogo, ,uliona hauwezi kufanya vitu vingi vikubwa kwasabu ulizoziona wewe na ukajitia moyo kwamba (siwezi )
MUNGU anamwambia Yeremia utaenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwakwe. Manake wewe Yeremia unasema hauwezi kuongea kwa akili zako, hauwezi kuongea kwa uwezo wako Ila kwa uwezo wa Mimi MUNGU utasema chochote nitakachokutuma na utafanya lolote nitakalokutuma.
MUNGU anamfundisha Yeremia kwamba; yaliyoshindikana kwako Yeremia hayakunishinda Mimi MUNGU , yaliyokwama kufanyika kwako kwa sababu ya umri wako mdogo , ukienda na Mimi utayafanya na makubwa kuliko umri wako, maana apa ulipo yeremia wewe ni nabii wa mataifa. Hallelujah. Hallelujah. Yeremia 1:6-8.
Ukisoma waamuzi 6: 11- 18 utamuona Gidion anatumwa na MUNGU akaokoe Israeli , Ila Gidion anaanza kujitetea kwamba yeye ni masikini na ni mdogo. MUNGU anamwambia Gidion ENENDA KWA UWEZO WAKO HUU. . BWANA anamwambia tena ya kuwa atakuwa pamoja naye. Sasa Gidion aliangalia umri wake akaangalia na uwezo wa kipato akajiona hawezi kufanya chochote . MUNGU anamwambia ulishindwa kwa uwezo wako ila ukienda na Mimi utaweza kutenda makuu, Gidion unaenda kuokoa Iraeli, wewe ni shujaa.💪
Mpenzi msomji, sijuhi unataka kufanya Nini ambacho unazani utashindwa, sikia nikwambie ; huu mwaka tunaenda na uwezo wetu huu Ila tunatenda makuu maana tunaenda sio peke yetu tena bali tunatenda na MUNGU mwenye uwezo wote.
Unataka kufanya biashara ENENDA KWA UWEZO WAKO HUU, unataka kusoma ENENDA KWA UWEZO WAKO HUU, unataka kujenga nyumba ENENDA KWA UWEZO WAKO HUU, unataka kufunga ndoa ENENDA KWA UWEZO WAKO HUU, unataka kufungua huduma ENENDA KWA UWEZO WAKO HUU, unataka kufanya chochote ENENDA KWA UWEZO WAKO HUU na MUNGU atakuwa pamoja nawe.
Chochote unachotaka kukifanya Kama utakubali kwenda na MUNGU nataka nikwakikishie kwamba utafanikiwa tuuuu.
Naitwa Loveness Audax
Tunaweza kuwasiliana kupitia WhatsApp number 0769412294
Pia unaweza kunipigia kwa number 0769412294.