بسم الله الرحمن الرحيم
Je, wewe ni mmoja wa watoto wema?
Amesema Allah (S.W) Hakuna wema mkubwa kama kuwatendea wema wazazi wawili.
﴿وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا
Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na (ameamuru)kuwatendea wema wazazi wawili.” (Surah Al-Isra, 17:23)
Tazama pia:
Surah Luqman – Aya ya 14 (31:14)
Au Surah An-Nisa – Aya ya 9 (4:9)
Ndugu zangu katika Imani.
Tumeandaa *Hauli ya Wazee Wetu* waliotangulia mbele ya haki. kuwafanyia du’a ya pamoja, sio wazazi wetu tu peke yake,lakini pia ndugu zetu Waislam Wakiume na Wakike, wote kwa pamoja.
Tumeazimia kuifanya Hauli hii kila mwaka Inshaallah, uwe ni muendelezo kwa kadri vile MOLA WETU MLEZI atakavyo tuafikia.
Na lengo jengine juu ya Jitihada hizi ni kumumba MOLA WETU MLEZI azibakishe iwe ni sehemu ya urith kwa vizazi vyetu na wao waliendeleze hili mpk kufikia vizazi na vuzazi vyao hapo baadae.
KWANINI TUOMBE HAYO!? HEBU TUTAFAKALI PAMOJA. JUU YA UCHACHE WA MIAKA 100 ILIOPITA NA MIAKA 100 BAADAE.
Nadhani tunaweza kukubaliana juu ya tafakali hii ya kwamba, Huenda ndani ya MIAKA 100 baadae, hakuna atakayebaki kwenye HIKI kizazi isipokuwa labda wale wachache waliochaguliwa na AllAH (S.W) kuwepo kufikia karne moja hapo baadae.
Lakini pia tukumbuke ya kwamba MIAKA 100 KABLA YETU, Bila shaka Palikuwa na watu waliokuwa wakiishi kwenye Jamii zetu au Miji
yetu hapo kabla na huenda hata kwenye Majumba tunayoishi sasa, walikuwa wakiishi miongoni mwao, Pengine ni mitaa tunayopita kwenda na kurudi kila siku za maisha yetu na wao walikuwa wakiipita pia,
Lakini leo hii hawapo tena na wengiwao historia imewafuta. kabisa kwenye kurasa zake hivyo hatuna tunachokijuwa juu yao isipokuwa wale wachache ambao walio acha ALAMA zisizofutika ndani ya KURASA za kitabu cha HISTORIA,
Watu ambao hawakuwa wabinafsi, WATU AMBAO WALIWAZA KUJENGA MISINGI IMARA YA KUSAIDIA SIO FAMILIA NA JAMII ZAO TU, HAPANA BALI WALILENGA KUWAFIKIA VIZAZI VYAO NA VIZAZI BAADA YAO,
Hawakuwaza kwajili ya Maslahi yao Binafsi. mpaka hii leo ATHALI zao zimetufikia na kutufikisha hapa tulipo, Ndio hao hao kwa kifupi bado tunaishi kupitia mifano na misingi bora ya maisha mema waliyoyatengeneza tangu hapo Awali..
HIVYO BASI MAAMUZI YETU YA LEO NDIO YATAKAYO TOA MWANGA WA KESHO YETU
MIAKA 100 ijayo ungependa HISTORIA IKUKUMBUKE WEWE KAMA NANI!?
je ulishawahi kufanya jambo hata dogo tu kwa mfano wa nukta moja tu, ambayo itaacha athali kwa vizazi na vizazi!?
Sio lazima kulifanya lenye mfano wa kama hili
tunalolifanya yapo mengi sana ambayo bado hayajafanywa ni kutazama na kutafakali
kwa kina juu ya hayo kama utaona ni yenye kukufaa.
Mwisho wa tafakali zangu kwa ufupi.
pia unaweza kushare zako kwenye
comment,
NA KAMA umeweza kusoma mpaka kufikia
hapa, basi nina imani huenda tukawa tupo
pamoja katika kulikamilisha hili, Na Tupo Tayari juianza Safari yetu hii, Ambayo tunaamini itakua ni sababu ya kuacha athali kwenye familia zetu, jamii zetu, vizazi vyetu na vyao hapo baadae, INSHAALLAH.
Basi, kwa machache hayo, inshaAllah, tumeazimia kufanya hauli hii: tarehe 10 / 10 / 2025. Inshaallah
Kama ALLAH (S.W) atatuafikisha kutimiza bajeti yetu tuliokusudia kwa muda muafaka, InshaAllah
Hauli yetu tutaifanya (Hadhala) Mtaa wa S/kuu na Kariakoo na wote mnakaribishwa.
Na kwa yoyote atakaye afikiwa na AllAH kutusapoti kwa namna yoyote ile basi karibu sana
mwasiliano ya haraka: WhatsApp: +255 714 43 00 44 unaweza kuwatumia ujumbe mfupi ma-admin wa
Facebook: @KARIAKOO FAMILY (We are Muslims Community) au @Al Mustakshif Abu Manal Danah
au @chyladolson. Hakuna zaidi ya hao wanao husika.
Asanteni wamaa alayna illal balaghul mubin.
Wasalaam Aleykum.
---