

# Event Details

- **Event Name**: WEKEZA MARATHONS
- **Event Start and End Date**: Sun, 20 Sep, 2026 at 01:00 pm (+03:00)
- **Event Description**: WEKEZA MARATHONS | WEKEZA MARATHONS

WEKEZA MARATHONS ni harakati ya kijamii, kielimu na kiafya inayolenga kuhamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa  kuthamini afya njema na kuwekeza kama njia endelevu ya kupambana na umaskini, kukuza ustawi wa kifedha, na kujenga mustakabali salama wa maisha.

 Kupitia mbio za marathon, WEKEZA MARATHONS hutumia michezo kama chombo cha kuamsha fikra, kuelimisha, na kuunganisha jamii katika safari ya mabadiliko ya kiuchumi.

WEKEZA MARATHONS imejengwa juu ya dhana kwamba umasikini hauondoki wenyewe, bali kwa kuukimbia kwa kufanya mabadiliko ya tabia, kuwekeza katika maarifa sahihi, na kufanya  uwekezaji wa kifedha wa muda mrefu. 

Mafanikio ya kifedha yanahitaji nidhamu, uvumilivu, maandalizi, na uamuzi wa kuanza safari bila kusubiri mazingira yawe kamili.

Dhana Kuu (Concept)
WEKEZA MARATHONS inatokana na falsafa kwamba uwekezaji ni safari ndefu hivyo mbio za marathon zinawakilisha safari ya maisha ya kifedha ambapo mshiriki hujifunza nidhamu,uvumilivu,kakabili changamoto, na kuendelea mbele hata pale anapochoka ili lengo lake litimie.

Kwa kutumia mbio kama lugha rahisi, WEKEZA MARATHONS huwasilisha elimu ya uwekezaji kwa namna inayoeleweka kwa wananchi wa kawaida, bila istilahi ngumu za kifedha, na kwa kuzingatia uhalisia wa maisha ya Watanzania.

Malengo ya WEKEZA MARATHONS:

Malengo makuu ya wekeza marathons ni kujenga utamaduni wa uwekezaji miongoni mwa Watanzania kwa kuunganisha afya ya mwili, elimu ya fedha, na mshikamano wa jamii katika mapambano dhidi ya umaskini.
Pamoja na hayo imedhamiria;
Kuelimisha jamii kuhusu misingi ya uwekezaji kwa lugha rahisi na mifano halisi.
Kuhamasisha wananchi kuanza kuwekeza hata kwa mtaji mdogo.
Kukuza uelewa wa tofauti kati ya akiba na uwekezaji.
Kujenga nidhamu ya kifedha na mtazamo wa muda mrefu.
Kuwezesha wananchi kuunganishwa na taasisi halali za uwekezaji.
Kukuza afya ya mwili na akili kama nguzo ya mafanikio ya kifedha.
Kuibua kizazi kinachotambua uwekezaji kama sehemu ya maisha ya kila siku.

MAANA YA KAULIMBIU YETU;
Kimbia Umasikini, Kimbilia Uwekezaji
(Run from Poverty. Run to Investment.)

“Kimbia Umasikini, Kimbilia Uwekezaji” ni wito wa mabadiliko ya fikra na vitendo.
Ni kauli mbiu inayohamasisha:
kukataa umaskini wa fikra na mazoea,
kuchukua hatua za makusudi kuelekea uwekezaji,
na kuanza safari ya kujenga uhuru wa kifedha.
Kauli mbiu hii inaunganisha moja kwa moja harakati za kimwili (kukimbia) na harakati za kiuchumi (kuwekeza), na kuifanya WEKEZA MARATHONS kuwa zaidi ya tukio na kuwa movement.

Kaa tayari kwa jambo hili adhimu.
Tarehe 20 mwezi wa 9 mwaka 2026,
Rasmi WEKEZA MARATHONS itafanyika.
Kutakua na Mbio za 5KM, 10KM na 21KM
Mafunzo mafupi ya elimu ya uwekezaji.
Ushauri wa kifedha wa moja kwa moja
Ushirikiano na taasisi mbalimbali za uwekezaji
Bila kusahau kupata connections na burudani.

Wekeza marathons imeratibiwa na Meza ya uwekezaji 
Tunawakaribisha wadhamini na washiriki katika kufanikisha tukio hili 💥💥💥

Mkurugenzi
Naytham S Masoud 
0746465095
- **Event URL**: https://allevents.in/dar-es-salaam/wekeza-marathons/200030367910731
- **Event Categories**: sports, marathons
- **Interested Audience**: 
  - total_interested_count: 48

## Ticket Details


## Event venue details

- **city**: Dar Es Salaam
- **state**: DS
- **country**: Tanzania
- **location**: Kisutu, Dar es Salaam
- **lat**: -6.8126901595954
- **long**: 39.279761657345
- **full address**: Kisutu, Dar es Salaam, Tanzania

## Event gallery

- **Alt text**: WEKEZA MARATHONS
  - **Image URL**: https://cdn-az.allevents.in/events4/banners/aa60440cb45e2412f2f6bb91dfd9f2bb3b927a84419d4a0f89d864f3a76efc19-rimg-w1080-h1010-dcf8f8f8-gmir?v=1787019392

## FAQs

- **Q**: When and where is WEKEZA MARATHONS being held?
  - **A:** WEKEZA MARATHONS takes place on Sun, 20 Sep, 2026 at 01:00 pm to Sun, 20 Sep, 2026 at 01:00 pm at Kisutu, Dar es Salaam, Tanzania.
- **Q**: Who is organizing WEKEZA MARATHONS?
  - **A:** WEKEZA MARATHONS is organized by Meza ya uwekezaji.
- **Q**: Who is this event for? Is it right for me?
  - **A:** WEKEZA MARATHONS is ideal for sports fans, athletes, fitness enthusiasts, and anyone who loves the thrill of live competitive action and the energy of a crowd. Whether you're a first-time attendee or a longtime enthusiast in Dar Es Salaam, this event is thoughtfully curated to deliver a standout experience worth every moment. If WEKEZA MARATHONS sounds like your kind of event, don't wait - spots fill up fast.

## Structured Data (JSON-LD)

```json
[
    {
        "@context": "https://schema.org",
        "@type": "Event",
        "name": "WEKEZA MARATHONS",
        "image": "https://cdn-az.allevents.in/events4/banners/aa60440cb45e2412f2f6bb91dfd9f2bb3b927a84419d4a0f89d864f3a76efc19-rimg-w1080-h1010-dcf8f8f8-gmir?v=1787019392",
        "startDate": "2026-09-20T13:00:00+03:00",
        "url": "https://allevents.in/dar-es-salaam/wekeza-marathons/200030367910731",
        "eventStatus": "https://schema.org/EventScheduled",
        "location": {
            "@type": "Place",
            "name": "Kisutu, Dar es Salaam",
            "address": {
                "@type": "PostalAddress",
                "streetAddress": "Dar es Salaam, Tanzania",
                "addressLocality": "Dar Es Salaam",
                "addressRegion": "DS",
                "addressCountry": "TZ"
            },
            "geo": {
                "@type": "GeoCoordinates",
                "latitude": "-6.8126901595954",
                "longitude": "39.279761657345"
            }
        },
        "eventAttendanceMode": "https://schema.org/OfflineEventAttendanceMode",
        "description": "WEKEZA MARATHONS | WEKEZA MARATHONS\n\nWEKEZA MARATHONS ni harakati ya kijamii, kielimu na kiafya inayolenga kuhamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa  kuthamini afya njema na kuwekeza kama njia endelevu ya kupambana na umaskini, kukuza ustawi wa kifedha, na kujenga mustakabali salama wa maisha.\n\n K",
        "organizer": [
            {
                "@type": "Organization",
                "name": "Meza ya uwekezaji",
                "url": "https://allevents.in/org/meza-ya-uwekezaji/28007924",
                "description": "Meza ya uwekezaji. 516 likes · 3 talking about this. MEZA YA UWEKEZAJI |THE INVESTMENTS TABLE \n\nTunakutanisha watu wa sekta zote kujifunza na kuwekeza..."
            }
        ]
    }
]
```